Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 2

Wana Waovu wa Eli

12 Wana wa Eli walikuwa watu waovu kabisa, hawakumheshimu Mwenyezi Mungu. 13 Basi ilikuwa desturi ya makuhani pamoja na watu kwamba kila mara yeyote anapotoa dhabihu na huku nyama ikiwa inachemshwa, mtumishi wa kuhani angekuja na uma wenye meno matatu mkononi mwake. 14 Angeutumbukiza huo uma kwenye sufuria au birika au sufuria kubwa au chungu, naye kuhani angejichukulia chochote uma ungekileta. Hivi ndivyo walivyowatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo. 15 Lakini hata kabla mafuta ya mnyama hayajachomwa, mtumishi wa kuhani angekuja na kusema kwa mtu aliyekuwa akitoa dhabihu, "Mpe kuhani nyama akaoke, kwani hatapokea nyama iliyochemshwa kutoka kwako, ila iliyo mbichi tu."

16 Mtu yule akimwambia, "Mafuta ya mnyama na yachomwe kwanza, ndipo uchukue chochote unachotaka," mtumishi angejibu, "Hapana, nipe sasa; kama hunipi, nitaichukua kwa nguvu."

17 Hii dhambi ya hawa vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa waliitendea dhabihu ya Mwenyezi Mungu kwa dharau.

Veja também