3 Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. 4 Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa, navyo vimelala kizingitini; ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.
6 Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu.