Publicidade

1 Samuel 6

Sanduku la Mungu larudishwa Israeli

1 Sanduku la Mwenyezi Mungu lilipokuwa limekaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba, 2 Wafilisti waliwaita makuhani wa Dagoni na waaguzi, na kuwaambia, "Tutafanya nini na hili Sanduku la Mwenyezi Mungu? Tuambieni jinsi tutakavyolirudisha mahali pake."

3 Wakajibu, "Kama mtalirudisha Sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe mikono mitupu bali kwa vyovyote mpelekeeni sadaka ya hatia. Kisha mtaponywa, nanyi mtafahamu kwa nini mkono wake haujaondolewa kwenu."

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-