Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Tessalonicenses 5

Kuweni tayari kwa siku ya Bwana

1 Basi ndugu, hatuna haja ya kuwaandikia kuhusu nyakati na majira, 2 kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Mwenyezi Mungu itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. 3 Watu wanaposema, "Kuna amani na salama," maangamizi huwajia ghafula, kama vile uchungu unavyomjia mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.

4 Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. 5 Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku.

Veja também

1 Tessalonicenses
Ver todos os capítulos de 1 Tessalonicenses