9 Lakini aliniambia, "Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu." Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Al-Masihi ukae juu yangu. 10 Hii ndiyo sababu nafurahia katika udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso na katika shida kwa ajili ya Al-Masihi. Kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu.
Publicidade
Publicidade