Publicidade

2 Coríntios 5

17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya. 18 Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kupitia kwa Isa Al-Masihi, na kutupatia sisi huduma ya upatanisho: 19 kwamba Mungu alikuwa ndani ya Al-Masihi akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. 20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Al-Masihi, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Al-Masihi: mpatanishwe na Mungu. 21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi5:21 au kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kupitia kwake Al-Masihi.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-