Msifungiwe nira pamoja na wasioamini
14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini. Kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 Kuna mapatano gani kati ya Al-Masihi na Beliari6:15 maana yake Uovu, yaani Shetani? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema:
"Nitakaa pamoja nao
na kutembea katikati yao,
nami nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu."
17 Kwa hiyo,
"Tokeni miongoni mwao,
mkatengwe nao,
asema Mwenyezi Mungu.
Msiguse kitu chochote kilicho najisi,
nami nitawakaribisha."