10 Kwa maana huzuni ya kiungu huleta toba iletayo wokovu, wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti. 11 Tazameni jinsi huzuni hii ya kiungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo.
Publicidade