Kupanda kwa ukarimu
6 Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye haba pia atavuna haba, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. 8 Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
10 Yeye ampaye mpanzi mbegu ya kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. 11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.