Kuponywa kwa maji
19 Watu wa mji wakamwambia Al-Yasa, "Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu anavyoona, lakini maji yake ni mabaya, na nchi haina mazao."
20 Akasema, "Nileteeni bakuli mpya, mweke chumvi ndani yake." Kwa hiyo wakamletea.
21 Kisha akaenda kwenye chemchemi na kuitupa ile chumvi ndani yake, akisema, "Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nimeyaponya maji haya. Kamwe hayatasababisha mauti tena wala kutozaa.’ " 22 Nayo yale maji yakaponywa hadi leo, sawasawa na neno la Al-Yasa alilokuwa amesema.