Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Wafalme 4

Mafuta ya mjane

1 Mke wa mmoja wa wana wa manabii akamlilia Al-Yasa, akamwambia, "Mtumishi wako, mume wangu, amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha Mwenyezi Mungu. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake."

2 Al-Yasa akamjibu, "Nitawezaje kukusaidia? Niambie, una nini ndani ya nyumba yako?"

Akasema, "Mtumishi wako hana kitu chochote kabisa, isipokuwa mafuta kidogo."

3 Al-Yasa akasema, "Zunguka kwa majirani zako wote ukaombe vyombo vitupu. Usiombe vichache. 4 Kisha ingia ndani na ujifungie mlango, wewe na wanao. Mimina mafuta kwenye vyombo vyote, na kila kimoja kinapojaa, kiweke kando."

5 Yule mjane akaondoka na kujifungia ndani, yeye na wanawe. Wao wakamletea vyombo, naye akaendelea kumimina mafuta. 6 Vyombo vyote vilipojaa, akamwambia mwanawe, "Niletee chombo kingine."

Lakini mwanawe akajibu, "Hakuna chombo kingine kilichobaki." Basi mafuta yakakoma kutiririka.

7 Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, "Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também