Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Wafalme 4:42-44

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Watu mia wanalishwa

42 Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutoka kwa nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Al-Yasa akasema, "Wape watu ili wale."

43 Mtumishi wake akamuuliza, "Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia moja?"

Lakini Al-Yasa akajibu, "Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Watakula na kusaza.’ " 44 Basi akaiandaa mbele yao ile mikate, wakala na baadhi yake wakasaza, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    42 1 Sam 9:4;1 Kor 9:11;Gal 6:6Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale. 43 Lk 9:13;Yn 6:9Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandalie hiki watu mia moja? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa BWANA asema hivi, Watakula na kusaza. 44 Mt 14:20;15:37;Yn 6:13;Mwa 18:14;Yer 32:17;Zek 8:6;Mt 19:26;Lk 1:37Basi akawaandalia, nao wakala, wakasaza, sawasawa na neno la BWANA.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    42 Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutokana na nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Elisha akasema, "Wape watu ili wale."

    43 Mtumishi wake akamuuliza, "Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia?"

    Lakini Elisha akajibu, "Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Watakula na kusaza.’ " 44 Basi akaiandaa mbele yao ile mikate, wakala na baadhi yake wakasaza, sawasawa na neno la Bwana.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.