Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Reis 5

Naamani aponywa ukoma

1 Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Mwenyezi Mungu alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ukoma.5:1 ukoma ni neno lililotumika kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi

2 Siku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimeenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani. 3 Akamwambia bibi yake, "Kama bwana wangu angemwona nabii aliye huko Samaria! Angemponya ukoma wake."

4 Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. 5 Mfalme wa Aramu5:5 yaani Shamu akamjibu, "Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli." Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi5:5 Talanta 10 za fedha ni sawa na kilo 340. za fedha, shekeli elfu sita za dhahabu5:5 Shekeli 6,000 za dhahabu ni sawa na kilo 70., na mavazi kumi. 6 Barua aliyopelekea mfalme wa Israeli iliandikwa hivi: "Pamoja na barua hii ninamtuma mtumishi wangu, Naamani, kwako ili uweze kumponya ukoma wake."

7 Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, "Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!"

8 Al-Yasa mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alikuwa amerarua mavazi yake, akamtumia ujumbe huu: "Kwa nini umerarua mavazi yako? Mwamuru mtu huyo aje kwangu, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli." 9 Kwa hiyo Naamani akaenda, akiwa na farasi wake na magari yake ya vita, na kusimama mlangoni mwa nyumba ya Al-Yasa. 10 Al-Yasa akamtuma mjumbe kumwambia, "Nenda uoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itapona, nawe utatakasika."

11 Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, "Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kupitisha mkono wake juu ya mahali penye ugonjwa ili aniponye ukoma wangu. 12 Je, Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko mito yoyote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga ndani ya hiyo mito na kutakasika?" Basi akageuka na kuondoka kwa hasira kuu.

13 Watumishi wa Naamani wakamwendea na kumwambia, "Baba yangu, kama huyo nabii angekuambia kufanya jambo lililo kubwa, je, hungelifanya? Je, si zaidi sana basi, anapokuambia, Oga na utakasike!’ " 14 Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo.

Veja também