15 Kesho yake asubuhi na mapema, mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka na kutoka nje, jeshi, pamoja na farasi na magari ya vita, likawa limeuzunguka mji. Mtumishi wake akasema, "Ole wetu, bwana wangu! Tutafanya nini?"
16 Nabii akajibu, "Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao."
17 Kisha Al-Yasa akaomba, "Ee Mwenyezi Mungu, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona." Ndipo Mwenyezi Mungu akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya vita yaliyowaka moto yamemzunguka Al-Yasa pande zote.