7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, "Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. 9 Kwa nini ulilidharau neno la Mwenyezi Mungu kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria Mhiti kwa upanga, na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni. 10 Basi kwa hiyo, upanga hautaondoka nyumbani mwako kamwe, kwa sababu ulinidharau mimi na kumchukua mke wa Uria Mhiti kuwa mkeo.’
13 Ndipo Daudi akamjibu Nathani, "Nimefanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu."
Nathani akamjibu, "Mwenyezi Mungu amekuondolea dhambi yako. Hutakufa. 14 Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za Mwenyezi Mungu kuonesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa."