10 Rispa binti Aya akachukua gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno hadi mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama mwitu wakati wa usiku. 11 Daudi alipoambiwa kile Rispa binti Aya, suria wa Sauli, alichokuwa amekifanya, 12 alienda akachukua mifupa ya Sauli na mwanawe Yonathani kutoka kwa watu wa Yabesh-Gileadi. (Walikuwa wameichukua kwa siri kutoka uwanja wa watu wote huko Beth-Shani, ambapo Wafilisti walikuwa wamewatundika baada ya kumuua Sauli huko Gilboa.) 13 Daudi akaileta mifupa ya Sauli na ya mwanawe Yonathani kutoka huko, pia mifupa ya wale waliokuwa wameuawa na kutupwa ilikusanywa.
14 Wakazika mifupa ya Sauli na ya mwanawe Yonathani katika kaburi la Kishi, babaye Sauli, huko Sela katika nchi ya Benyamini, nao wakafanya kila kitu mfalme alichoagiza. Baada ya hayo, Mungu akajibu maombi kwa ajili ya nchi.
Vita dhidi ya Wafilisti
(1 Nyakati 20:4-8)