5 na kutoka kwa Isa Al-Masihi, aliye shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, mtawala wa wafalme wa dunia.
Kwake yeye anayetupenda na aliyetuweka huru kutoka dhambi zetu kwa damu yake, 6 na akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, ili tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba1:6 Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi. yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.