Mwana-Kondoo na wale 144,000
1 Kisha nikatazama, na hapo mbele yangu Mwana-Kondoo alikuwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale elfu mia moja na arobaini na nne wenye jina la Mwana-Kondoo na jina la Baba14:1 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. yake limeandikwa kwenye paji za nyuso zao. 2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kwa kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao. 3 Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi, na mbele ya wale viumbe wanne wenye uhai, na wale wazee. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao elfu mia moja na arobaini na nne waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. 4 Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni bikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5 Vinywani mwao hapakuonekana uongo, wala hawakuwa na hatia yoyote.