Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 21:1-3

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Mbingu mpya na nchi mpya

1 Kisha nikaona "mbingu mpya na nchi mpya", kwa maana mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwa na bahari tena. 2 Nikauona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe. 3 Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, "Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Isa 65:17;66:22;2 Pet 3:13;Ufu 20:11Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hakuna bahari tena. 2 Isa 52:1;61:10;Ufu 3:12;19:17;Ebr 11:10Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Eze 37:27;Law 26:11-12;Zek 2:10;Isa 8:8Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.21:3 Au hivi, Naye mwenyewe, Mungu pamoja nao, atakuwa Mungu wao.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena. 2 Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe. 3 Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, "Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.