2 Yeye na jamaa yake yote walikuwa wacha Mungu; alitoa kwa ukarimu kwa wale walio na mahitaji na kumwomba Mungu mara kwa mara.
15 Ile sauti ikasema naye mara ya pili, "Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa."
28 Akawaambia, "Mnajua kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi.
Hotuba ya Petro
34 Ndipo Petro akafungua kinywa chake akasema, "Mungu hana upendeleo, 35 lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye.
Watu wa mataifa wapokea Roho wa Mungu
44 Petro alipokuwa akisema maneno haya, Roho Mtakatifu wa Mungu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe.