Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 12:7-10

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

7 Ghafula malaika wa Mwenyezi Mungu akatokea, na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, "Ondoka upesi!" Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.

8 Yule malaika akamwambia, "Vaa nguo zako na viatu vyako." Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, "Jifunge vazi lako na unifuate." 9 Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono. 10 Walipita kundi la kwanza la walinzi na la pili, wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo, wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    7 Mdo 5:19Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. 8 Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. 9 Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. 10 Na walipopita kundi la walinzi wa kwanza na wa pili, wakafika hadi mbele ya lango la chuma la kuingilia mjini, nalo lango likawafungukia lenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    7 Ghafula malaika wa Bwana akatokea na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, "Ondoka upesi!" Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.

    8 Yule malaika akamwambia, "Vaa nguo zako na viatu vyako." Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, "Jifunge vazi lako na unifuate." 9 Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono. 10 Wakapita lindo la kwanza na la pili, ndipo wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.