Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 16:1-5

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Timotheo aungana na Paulo na Sila

1 Paulo akafika Derbe na kisha Listra, ambako kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, ambaye mama yake alikuwa Myahudi aliyeamini, lakini baba yake alikuwa Myunani. 2 Alikuwa amesifiwa sana na wale ndugu waliokuwa wameamini huko Listra na Ikonio 3 Paulo alitaka Timotheo aandamane naye, hivyo akamtahiri kwa sababu ya Wayahudi walioishi eneo lile, kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani. 4 Walipokuwa wakienda mji kwa mji, wakawa wanawapa maamuzi yaliyotolewa na mitume na wazee huko Yerusalemu ili wayafuate. 5 Hivyo makundi ya waumini yakaimarika katika imani, na wakaongezeka kwa idadi kila siku.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mdo 17:14;19:22;2 Tim 1:5;Flp 2:19-22Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Mgiriki. 2 Mdo 6:3Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. 3 Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Mgiriki.

    4 Mdo 15:23-29Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. 5 Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Paulo akafika Derbe na kisha Listra, ambako kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, ambaye mama yake alikuwa Myahudi aliyeamini, lakini baba yake alikuwa Myunani. 2 Alikuwa amesifiwa sana na wale ndugu waliokuwa wameamini huko Listra na Ikonio 3 Paulo alitaka Timotheo afuatane naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwa wanaishi eneo lile kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani. 4 Walipokuwa wakienda mji kwa mji, wakawa wanawapa maamuzi yaliyotolewa na mitume na wazee huko Yerusalemu ili wayafuate. 5 Hivyo makanisa yakawa imara katika imani na kuongezeka kiidadi kila siku.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.