Kushuka kwa Roho wa Mungu
1 Siku ya Pentekoste ilipowadia, waumini wote walikuwa mahali pamoja. 2 Ghafula, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali ikatoka mbinguni, ikaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3 Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
5 Basi walikuwako Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu.