Pular para o conteúdo
Publicidade

Atos 2

41 Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa, na siku ile waliongezeka watu wapatao elfu tatu.

Ushirika wa waumini

42 Nao wakadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Waumini wote walikuwa mahali pamoja, nao wakashirikiana katika mambo yote. 45 Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu2:46 Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu., wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa.

Veja também