Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 22:25-28

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wampige mijeledi, Paulo akamwambia kiongozi wa askari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, "Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumpiga mtu ambaye ni raia wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?"

26 Yule kiongozi aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari na kumwambia, "Unataka kufanya nini? Kwa maana huyu mtu ni raia wa Rumi."

27 Yule jemadari akaja akamuuliza Paulo, "Niambie, wewe ni raia wa Rumi?"

Paulo akajibu, "Naam, hakika."

28 Ndipo yule jemadari akasema, "Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu."

Paulo akasema "Lakini mimi ni raia wa Rumi kwa kuzaliwa."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    25 Mdo 16:37;23:27Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule ofisa aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado? 26 Yule jemadari aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi. 27 Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. 28 Jemadari akajibu, Mimi nilipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia kiongozi wa askari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, "Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumchapa mtu ambaye ni raiya wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?"

    26 Yule kiongozi aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari na kumwambia, "Unataka kufanya nini? Kwa maana huyu mtu ni raiya wa Rumi."

    27 Yule jemadari akaja akamuuliza Paulo, "Niambie, wewe ni raiya wa Rumi?"

    Paulo akajibu, "Naam, hakika ndiyo."

    28 Ndipo yule jemadari akasema, "Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu."

    Paulo akasema "Lakini mimi ni raiya wa Rumi kwa kuzaliwa."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.