9 Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi6:9 Nyumba ya ibada na mafunzo. la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa) la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na jimbo la Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano.
11 Ndipo kwa siri wakawashawishi watu fulani waseme, "Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kufuru dhidi ya Musa na dhidi ya Mungu."