Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 8

18 Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho wa Mungu mitume walipoweka mikono juu yao, akataka kuwapa fedha 19 akisema, "Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apate kupokea Roho wa Mungu."

20 Petro akamjibu, "Fedha yako na iangamie pamoja nawe, kwa sababu ulidhani unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha! 21 Wewe huna sehemu wala fungu katika huduma hii kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. 22 Kwa hiyo tubu kwa uovu huu wako na umwombe Mwenyezi Mungu. Yamkini aweza kukusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako. 23 Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi."

24 Ndipo Simoni akajibu, "Niombeeni kwa Mwenyezi Mungu, ili hayo mliyosema lolote lisinitokee."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também