5 Filipo akaenda mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Al-Masihi8:5 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta.. 6 Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza alizofanya, wakasikiliza kwa makini yale aliyosema. 7 Pepo wachafu wakawa wakiwatoka watu wengi huku wakipiga kelele, na wengi waliopooza na viwete wakaponywa. 8 Hivyo pakawa na furaha kuu katika mji huo.