Pular para o conteúdo
Publicidade

Daniel 1

Mafunzo ya Danieli huko Babeli

1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja akazingira Yerusalemu. 2 Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza, pamoja na baadhi ya vyombo kutoka Hekalu la Mungu. Nebukadneza akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari1:2 yaani Babeli, naye akaviweka nyumbani ya hazina ya mungu wake.

3 Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa mfalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya mfalme na kutoka jamaa kuu: 4 vijana wa kiume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonesha kipaji katika kila aina ya elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo. 5 Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, na hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme.

6 Baadhi ya hawa vijana walitoka Yuda: Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria.

Veja também