3 Kwa hiyo nikamgeukia Mwenyezi Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, na kuvaa gunia na kujipaka majivu.
4 Nikamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, na kutubu:
"Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake, 5 tumetenda dhambi na kufanya mabaya. Tumekuwa waovu na tumeasi; tumegeuka mbali na maagizo yako na sheria zako.
Majuma sabini
20 Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,