16 Nami wakati ule nikawaagiza waamuzi wenu: "Sikilizeni magomvi kati ya ndugu zenu na mwamue kwa haki, hata kama shauri ni kati ya ndugu Waisraeli, au kati ya mmoja wa ndugu Mwisraeli na mgeni. 17 Msioneshe upendeleo katika maamuzi; wasikilizeni wote sawasawa, wadogo kwa wakubwa. Msimwogope mtu yeyote, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Mniletee mimi shauri lolote lililo gumu sana kwenu, nami nitalisikiliza."
Publicidade