Mche Mwenyezi Mungu
12 Na sasa, ee Israeli, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, anataka nini kwako ila kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, 13 na kuyashika maagizo ya Mwenyezi Mungu na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?