Pular para o conteúdo
Publicidade

Deuteronômio 11

18 Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu. 19 Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni mnapoketi nyumbani na mnapotembea njiani, mnapolala na mnapoamka. 20 Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu, 21 ili siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ile Mwenyezi Mungu aliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.

Veja também