Zaka
22 Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka. 23 Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo na mbuzi mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili mpate kujifunza kumheshimu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, daima. 26 Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ng’ombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na watu wa nyumbani mwenu mtaila mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kufurahi.
28 Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu, 29 ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.