Mafanikio baada ya kumgeukia Mwenyezi Mungu
1 Baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakapokutawanya miongoni mwa mataifa, 2 hapo wewe na watoto wako mtakapomrudia Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo, 3 ndipo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka mataifa yote kule alikutawanya. 4 Hata kama umefukuziwa katika nchi ya mbali kiasi gani chini ya mbingu, kutoka huko Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakukusanya na kukurudisha. 5 Yeye Mwenyezi Mungu atakurudisha katika nchi iliyokuwa mali ya baba zako, nawe utaimiliki. Naye atakufanya ufanikiwe sana na kukuzidisha kwa idadi kuliko baba zako. 6 Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi.