Kufanywa hai ndani ya Al-Masihi
1 Ninyi mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, 2 ambazo mlizitenda mlipofuata njia za ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii. 3 Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulistahili ghadhabu, kama watu wengine wote.