Wamoja katika Al-Masihi
11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo awali ninyi ambao ni watu wa Mataifa kwa kuzaliwa na kuitwa "wasiotahiriwa" na wale wanaojiita "waliotahiriwa" (yaani tohara ifanyikayo katika mwili kwa mikono ya wanadamu), 12 kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi hamkuwa na tumaini wala Mungu duniani. 13 Lakini sasa katika Al-Masihi Isa, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kupitia kwa damu ya Al-Masihi.