Pular para o conteúdo
Publicidade

Waefeso 4:1-12

Umoja katika mwili wa Al-Masihi

1 Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana Isa, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa. 2 Kwa unyenyekevu wote na upole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo. 3 Jitahidini kudumisha umoja wa Roho wa Mungu katika kifungo cha amani. 4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo4:5 Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali. Wafuasi wa Isa Al-Masihi pia wanapokea Roho wa Mungu kama dhibitisho ya imani yao. mmoja, 6 Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.

7 Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Al-Masihi. 8 Kwa hiyo husema:

"Alipopaa juu zaidi,

aliteka mateka,

akawapa wanadamu vipawa."

9 (Asemapo "alipaa juu," maana yake nini isipokuwa ni kusema kwamba Al-Masihi pia alishuka pande za chini sana za dunia4:9 pande za chini sana za dunia hapa maana yake Kuzimu? 10 Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu zaidi kupita mbingu zote, ili apate kuujaza ulimwengu wote.) 11 Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili mwili wa Al-Masihi upate kujengwa

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.