14 Basi hatutakuwa tena watoto wachanga, tukiyumbishwa na mawimbi, na tukipeperushwa hapa na pale na kila upepo wa mafundisho, na kwa ujanja na hila za watu katika njama zao. 15 Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani Al-Masihi. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, huku kila kiungo kikifanya kazi yake.
Waefeso 4:14-16
Em outras traduções
- SRUV Swahili Revised Union Version
14 1 Kor 14:20;Ebr 13:9ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Efe 1:22;5:23;Kol 1:18Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16 Kol 2:19Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
14 Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu. 15 Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani, Kristo. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikamanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.