Mordekai anapewa heshima
1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi, hivyo akaagiza aletewe kitabu cha kumbukumbu za matukio ya utawala wake, asomewe. 2 Ikaonekana imeandikwa humo kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero.
3 Mfalme akauliza, "Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?"
Watumishi wake wakajibu, "Hakuna lolote alilotendewa."
6 Hamani alipoingia, mfalme alimuuliza, "Afanyiwe nini mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu?"
Basi Hamani akawaza moyoni mwake, "Ni nani mwingine ambaye mfalme angemheshimu kuliko mimi?"
10 Mfalme akamwamuru Hamani, "Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri."
11 Hivyo Hamani akachukua joho na farasi. Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi, akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, "Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!"