11 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, 12 "Nimesikia manung’uniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ "
13 Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na utando wa umande kuzunguka kambi. 14 Umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya mchanga wa jangwa. 15 Waisraeli walipoona, wakaambiana, "Hiki ni nini?" Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Musa akawaambia, "Huu ndio mkate ambao Mwenyezi Mungu amewapa mle.