Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 17:9,11-13,15

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

9 Musa akamwambia Yoshua, "Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu."

11 Ikawa wakati wote Musa alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. 12 Mikono ya Musa ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Haruni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Musa, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti hadi jua lilipozama. 13 Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga.

15 Musa akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi17:15 maana yake Mwenyezi Mungu ni Bendera yangu.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 Mdo 7:45;Ebr 4:8Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, uende ukapigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. 11 Yak 5:16Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. 12 Lakini mikono ya Musa ililegea; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitengemaza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. 13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. 15 Amu 6:24Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;17:15 Maana yake ni Bwana wangu au Mungu wangu ni Bendera yangu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    9 Mose akamwambia Yoshua, "Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu."

    11 Ikawa wakati wote Mose alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. 12 Mikono ya Mose ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Aroni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Mose, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama. 13 Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga.

    15 Mose akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi.17:15 Yehova Nisi maana yake ni Bwana ni Bendera yangu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.