Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 2

5 Ndipo binti Farao akateremka kwenye Mto Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti Farao akaona kisafina kwenye matete, akamtuma mmoja wa wajakazi wake kukichukua. 6 Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, "Huyu ni mmoja wa watoto wa Waebrania."

7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, "Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Waebrania akulelee huyu mtoto?"

8 Binti Farao akamjibu, "Ndiyo, nenda." Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, "Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa." Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea.

Veja também