Pular para o conteúdo
Publicidade

Êxodo 20

3 "Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 5 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanaonichukia, 6 lakini ninaonesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaonipenda na kuzishika amri zangu.

7 Usilitaje bure jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa kuwa Mwenyezi Mungu hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. 9 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 10 lakini siku ya saba ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Kwa kuwa kwa siku sita, Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.

12 Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Mwenyezi Mungu, Mungu wako.

13 Usiue.

14 Usizini.

15 Usiibe.

16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako."

Veja também