6 Musa akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli, na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. 7 Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, "Tutafanya kila kitu alichosema Mwenyezi Mungu, nasi tutatii."
8 Ndipo Musa akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, "Hii ni damu ya agano ambalo Mwenyezi Mungu amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote."