Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 26:1,7,14,15,31,33

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Maskani ya Mungu

1 "Tengeneza maskani ya Mungu kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo.

7 "Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika Maskani. 14 Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo26:14 pengine ni mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.

15 "Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani ya Mungu.

31 "Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia. 33 Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Kut 25:9;29:42,43;40:2,17;Mdo 7:44,45;Ebr 8:2-5;9:2-11;Ufu 21:3;1 Kor 12:28;Efe 4:11,12;Ebr 1:14Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.

    7 Kut 36:14Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja. 14 Kut 36:19;Hes 24:5Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.

    15 Nawe fanya hizo mbao za maskani za mti wa mjohoro, zenye kusimama.

    31 Law 16:2;2 Nya 3:14;Mt 27:51;Mk 15:38;Lk 23:45;Ebr 9:3Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; 33 Ebr 6:19;9:3-5;Kut 25:16;40:21;Yos 4:11;1 Sam 4:6;6:19;1 Fal 8:6;1 Nya 15:1;Ufu 11:19;Law 16:2;Mt 24:15Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 "Tengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo.

    7 "Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. 14 Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.26:14 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.

    15 "Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani.

    31 "Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia. 33 Ningʼiniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.