17 Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 18 katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 19 safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 20 na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. 21 Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.
Kutoka 28:17-21
Em outras traduções
- SRUV Swahili Revised Union Version
17 Kut 30:10;Mal 3:17Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza; 18 na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi; 19 na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto; 20 na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, shohamu na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake. 21 Hes 1:5;2:3;Ufu 7:4-8;21:12Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa mihuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hayo makabila kumi na mawili.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
17 Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 18 katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 19 safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 20 na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. 21 Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.