13 Musa akamwambia Mungu, "Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani?’ Nitawaambia nini?"
14 Mungu akamwambia Musa, "Mimi niko ambaye niko3:14 au Nitakuwa kama Nitakavyokuwa; au, Mimi Ndiye. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘Mimi niko amenituma kwenu.’ "