Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 32:11-14,32,33

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

11 Lakini Musa akamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wake, akasema, "Ee Mwenyezi Mungu, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu? 12 Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako. 13 Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote niliyowaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ " 14 Kisha Mwenyezi Mungu akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia.

32 Lakini sasa nakusihi, wasamehe dhambi yao; lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kitabu ulichoandika."

33 Mwenyezi Mungu akamjibu Musa, "Yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kitabu changu.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Hes 14:13-19;Kum 9:18,26-29;Zab 74:1;106:23Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? 12 Kwa nini Wamisri waseme, kuwa "Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?" Geuza katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako. 13 Mwa 22:16-17;12:7;13:15;35:12;17:8;Ebr 6:13Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele. 14 Hes 23:19;Kum 32:36;2 Sam 24:16;1 Nya 21:15;Yer 18:8;Hos 11:8;Yoe 2:13;Yn 3:10Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.

    32 Zab 69:29;Ufu 3:5;22:19;Kum 9:14;Rum 9:3;Zab 56:8;139:16;Flp 4:3Lakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. 33 Law 23:30;Eze 18:4BWANA akamwambia Musa, Mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    11 Lakini Mose akamsihi Bwana Mungu wake, akasema, "Ee Bwana, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu? 12 Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako. 13 Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ " 14 Kisha Bwana akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia.

    32 Lakini sasa nakusihi, wasamehe dhambi yao; lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kwenye kitabu ulichoandika."

    33 Bwana akamjibu Mose, "Yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kwenye kitabu changu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.