6 Mwenyezi Mungu akapita mbele ya Musa, akitangaza, "Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, 7 akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne."
Kutoka 34:6,7
Em outras traduções
- SRUV Swahili Revised Union Version
6 Kut 20:5-6;Hes 14:18;Kum 5:9-10;7:9-10;Neh 9:17;Yoe 2:13;Rum 2:4;Zab 108:4BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 Yer 32:18;Dan 9:4;Efe 4:32;1 Yoh 1:9;Yos 24:19;Ayu 10:14mwenye kuwaonea huruma watu maelfu,34:7 maelfu au maelfu ya vizazi. mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
6 Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, "Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, 7 akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.